Tuesday , 25th Jul , 2023

Rais William Ruto amesema kuwa yupo tayari kuonana na Raila Odinga  kwa mazungumzo ya ana kwa ana ila kwa sasa yupo nchini Tanzania na Kesho jioni atatejea Kenya

Ruto amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kueleza nia yake hiyo ya kuonana na Odinga

“Rafiki yangu Raila Odinga nipo Tanzania kwa ajili ya mkutano wa Rasilimali watu ili kuoanisha upanuzi wa nafasi za ajira katika bara letu. Nitarudi kesho jioni, na kama ulivyokuwa ukijua, ninapatikana na niki tayari  kwa mazungumzo ya ana kwa ana  wakati wowote kwa urahisi” Anaandika Rais Ruto.

Itakumbukwa mapema leo mchana Raila Odinga alizungumza na wanahabari na kusema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alienda nchini Kenya Kwa ajili ya kuwapatanisha lakini Rais Ruto alikwamisha jitihada hizo.