
Picha kwa hisani ya Mtandao
Kwa mujibu wa chapisho la Benki ya Dunia mwaka 2022 kuhusu hali ya kujifunza duniani, inasema licha ya nchi hizo kupiga hatua kubwa zaidi za kimaendeleo kwa miongo miwili ikiwa ni pamoja na kujenga shule na kuboresha mazingira ya elimu lakini bado mfumo wa elimu wa Nchi hizo hautoi nafasi ya watu kujifunza.na kwa hivi sasa tatizo ni kubwa zaidi kuliko iliyokuwa miaka ya nyuma wakati majengo ya shule na mazingira ya elimu yalikuwa mabaya zaidi.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Phillip Mpango wakati akifungua mkutano wa mawaziri wa Afrika katika kutatua changamoto ya hali ajira kwa vijana anasema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa katika kushughulikia wasiwasi wa idadi ya watu kwa kufanya uwekezaji mzuri katika afya ya watu ,na kuporesha hali ya elimu kwa kiwango cha juu ambayo ndio inawapa vijana ujuzi na ujuzi unaohitajika kwa mafanikio ya kiuchumi ya nchi za Afrika.
"Inakadiriwa kuwa umaskini wa kujifunza utaongezeka kwa asilimia 10 hadi zaidi ya asilimia 60 katika nchi zinazoendelea duniani kote na kutoka asilimia 83 hadi zaidi ya asilimia 90 katika nchi maskini zaidi duniani na hivyo hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ili kushugulikia ili kutatua changamoto hii".Amesema Dkt Mpango.
Tanzania inafanya nini kukabiliana na hali hii?
Hivi sasa Tanzania ipo katika mchakato wa kupitia upya sera ya elimu ya mwaka 2014,ikiwa ni pamoja na kupitia sharia ya Elimu na Mitaala na mapitio hayo yanalenga kuboresha mfumo wa elimu ya ufundi utakaozingatia ujuzi wa mikono,uwezo wa kujenga mawazo mazuri na kuangalia elimu ambayo itatazama vipaji kwa watoto
Inaelezwa kuwa matarajio ni kuwa mchakato huo utasaidia kuongeza tija kwa vijana,ushindani katika soko la pamoja la ajira na kuwaandaa wahitimu kuwa wabunifu wa kazi na sio wanaotafuta kazi.
Wadau wanasemaje kuhusu mfumo wa sasa?
Moja ya wadau wa elimu nchini Tanzania Richard mabala katika moja ya mahojiano na East Afrika radio anasema mfumo wa elimu wa Tanzania umekuwa ukimuandaa motto kwa ajili ya Mtihani kwa maana ya kukaririsha zaidi kuliko kumuandaa muhitimu kuingia kwenye ushindani wa soko la ajira.
Mabara aliongeza kuwa Mwanafunzi wa Tanzania anatumia muda mwingi kukariri vitu ambavyo hatakutana navyo akiingia kwenye ajira na hata baadhi ya mada zinazofundishwa kwenye mitaala haiendani na soko la ajira kwa sasa.