
Akizungumza na waandishi wa habari jumanne ya Leo Julai 25, 2023 Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmedy Ally amesema ni mchezo ambao watautumia katika kuwaonyesha Wanachama na Mashabiki wao kikosi chao cha kuwaletea ubingwa msimu 2023 -2024 katika mashindano ambayo wanashiriki.
'' Timu hii ya Power Dynamo wanashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa msimu ujao hivyo wanacheza na timu kubwa ambayo inaweza kutoa changamoto kwa wachezaji wetu”amesema Ahmedy.
kwa upande mwingine mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kutoka Dar es salaam wamewapongeza viongozi wao kwa kufanya usajili mzuri na wakiwataka wapenzi wa soka wajitoke kwa wingi uwanja kushuhudia wachezaji wao.
Kikosi cha Simba Sc kimeweka kambi ya wiki tatu nchini Uturuki tokea Julai 12, 2023 kwaajili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi 2023/24.