
Wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.
Barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka katika hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita 2023.
Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia barabara hiyo kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo