
Chongolo ameeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliokutanisha maelfu ya wakazi wa kanda ya Kaskazini hususani mikoa ya Arusha,Manyara na kilimanjaro ambapo amebainisha kuwa ni hatua ya makusudi kwa Serikali kuzifungua fursa za uwekezaji katika sekta ya bandari na kuonesha upana wa manufaa yaliyopo katika Sekta hiyo.
"Nisisitize wataalamu na wajuzi wa sheria ambao wana maoni na ushauri wa kubadilisha baadhi ya vingele vya sharia vikaleta tija zaidi ya vilivyo sasa waje mezani ili tuboreshe zaidi tukiwa na kitu kinachoenda kuongeza tija kwenye nchi yetu na si vinginevyo na sio kutunga uongo na kuwa na kuwagombanisha wananchi na Serikali yao"-Amesema Chongolo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa uchukuzi Atupele Mwakibete amefafanua kuwa ubora wa miundombinu ya bandari ya Dar es Salaam kwa sasa hauendani na uhitaji na ushindani uliopo na hivyo serikali kuchukua hatua ya kutafuta namna bora itakayosaidia kuongeza thamani ya huduma zinazotolewa na badari hiyo.
‘’Biashara ya bandari ya ushindani na kati ya mataifa makubwa ambayo tunafanya nayo kazi ni kutoka Kongo mzigo wake ni asilimia 41%, Uganda ni 2% peke yake,Rwanda ni 28% ukienda Zambia ni 23% ya mzigo wote tafsiri yake ni nini,hawa ambao tunafanya nao biashara baada ya kuona bandari yetu ya Dar es salaam wameanza kutafuta njia mbadala kupeleka mizigo yao”-Amesema Mwakibete.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kudumu ya Uwekezaji na mitaji ya Umma na Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa amechukua wasaa huo kuwataka watanzania kutoziafiki taarifa ambazo anazitaja kuwa si sahihi juu ya kuuzwa kwa bandari.
"Lipo swali kubwa ambapo nadhani hapa ndio msingi wa mkutano wetu,wako watanzania wanaojiuliza,je bandari imeuzwa? Wako watu wanajiuliza, je bandari zetu zimeuzwa,jibu lake ndugu zangu ni hapana"-Amesema Silaa.
Mkutano huo wa hadhara umefanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa lengo ni kutoa ufafanuzi juu ya hatua mbalimbali zinazogusa utekelezaji wa ilani wa chama hicho.