Friday , 21st Jul , 2023

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia kwa mahojiano Mohammed Jabir mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Kiislamu ya Qiblatain iliyopo Kawe kwa tuhuma za mauaji ya Mwalimu wake (Patron) Hassan Mohammed (21)

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumane Muliro

Tukio hilo limetokea jana Julai 20, 2023, majira ya saa 11 alfajiri baada ya mwalimu huyo kuwaamsha wanafunzi kwa ajili ya ibada ya asubuhi na kwamba mtuhumiwa alikaidi na baada ya wenzake kuondoka alimchoma kisu mwalimu huyo.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Jumanne Muliro amesema Mwalimu huyo alipoteza maisha ambaye alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mwananyamala na mwanafunzi huyo atafikishwa mahakamani haraka iwekenavyo.