Monday , 17th Jul , 2023

Watu watatu wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Isima, Kata ya Nyakagomba mkoani Geita, wamejeruhiwa na vitu vyenye ncha kali na watu wasiojulikana na kuiba magunia mawili ya Mahindi.

Watatu wa familia moja waliojeruhiwa na wasiojulikana

Tukio hilo la kuvamiwa kwa familia hiyo limetokea jana majira ya asubuhi ambapo wavamizi waliingia kwenye nyumba na kuchukua magunia ambapo baada ya mama mwenye mji kupiga kelele ndipo walipoanza kumpiga kila aliekuja kutoa msaada.

Wakiongelea tukio hilo ndugu wa majeruhi wanasema wavamizi hao walijitambulisha kuwa wao ni maafisa wa polisi ambao waliingia ndani kwa dhumuni la kusaka bangi.

Mhudumu wa Hospitali ya halmashauri ya Mji Geita, Emmanuel Gidioni, amekiri kupokea majeruhi hao ambao hali zao kwa sasa zinaendelea vizuri.

Akiongea kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amekiri kupokea taarifa hizi huku akiliagiza jeshi la Polisi kuchunguza tukio hilo.