Gari lililopata ajali
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 12:07 alfajiri katika eneo la Mzibira wilayani Bukombe na kudai licha ya dereva wa gari iliyokuwa imebeba abiria kuwa mwendokasi lakini pia alisinzia.
Kamada Jongo amesema gari hiyo ya abiria iliyokuwa inatokea wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga kwenda Nyakanazi wilayani Biharamulo imegongana uso kwa uso na lori hilo lililokuwa linatoka Nyakanazi kwenda Kahama huku dereva wa gari dogo na kondakta wake wakifariki pamoja na abiria wengine wanne.