Thursday , 13th Jul , 2023

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amewataka viongozi mkoani humo kuhakikisha wanawatumikia ipasavyo wananchi na wanatatua kero zao kwani hawahitaji swaga zao bali kazi na maendeleo.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Akizungumza katika ziara yake wilayani Kiteto, pamoja na mambo mengine ameonya viongozi haswa wa vijiji kwa kutoita mikutano ya kisheria ya vijiji na kusababisha malalamiko

"Nitakapopita tena kwenye maeneo yenu ya vijiji, nikute mmefanya mikutano ya kijiji kwa kijiji, hawa wananchi ndio wanaotufanya tuitwe viongozi wa mkoa, bila wao hakuna Mtendaji wala Mwenyekiti atakayekuwa na thamani," amesema RC Sendiga.