Saturday , 8th Jul , 2023

Kitabu kiitwacho Africa Magufuli na Badiliko kilichoandikwa na Profesa Malango Chinthenga wa Malawi kimetajwa kuvutia nchi nyingi za Afrika Mashariki zikiwamo Tanzania na Kenya huku Watanzania wakiwa tayari kukitafsiri kwa Kiswahili.

Kitabu hicho ambacho kilizinduliwa mwezi uliopita mjini Lilongwe na mwandishi huyo ambaye anaelezea namna ambavyo Afrika inaweza kuendelea na hatua ambazo Tanzania ilipiga chini ya uongozi wa Rais hayati John Pombe Magufuli  kiuchumi na kiuongozi.

Profesa Chinthenga,  amefichua kwamba, amesaini mkataba na wachapishaji wa vitabu wa TPH wa kuuza kitabu hicho nchini Tanzania na pia ameingia makubaliano na kitivo cha lugha cha Chuo Kikuu cha Mbeya cha Sayansi na Teknolojia ili kitabu hicho kitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili.