Tuesday , 4th Jul , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Lindi, linamshikilia Jalina Liwajila (42) mkazi wa Kijiji cha Rutamba mkoani humo ambaye hujulikana kwa shughuli zake za uganga wa kienyeji kwa kosa la kumuunguza moto mgongoni mtoto mwenye umri wa miaka 9 kwa madai ya kuwa alikuwa akimtibu degedege.

Mgongo ulioungua

Inaelezwa kuwa mtoto huyo alikuwa akipatiwa matibabu kwa kulazwa kwenye kitanda cha kienyeji (kitanda cha kamba) ambapo chini yake kulikuwa na moto unaochemsha maji kwenye Sufuria, maji ambayo yalitoa mvuke mkali na kumfikia mtoto huyo wa darasa la kwanza na kumuunguza eneo la mgongoni.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi ACP Pili Mande, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kuendelea kumshikilia Jalina Liwajila (mganga wa kienyeji) kwa mahojiano zaidi