Sunday , 2nd Jul , 2023

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde, amekabidhi mashamba ekari 4 mahsusi kwa kilimo cha mbogamboga na matunda kwa vikundi vya wafanyabiashara wadogo wa Twiga Group soko la Sabasaba na Mavunde garden soko kuu Majengo Jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde

Mavunde amefanya makabidhiano hayo ya mashamba kwa vikundi hivyo katika mbuga ya Sogeambele, Kata ya Chihanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi.

"Ni imani yangu kupitia mashamba haya mtaweza kuzalisha kwa wingi mazao ya mbogamboga na matunda na mkawa wasambazaji wakubwa wa mazao hayo ndani na nje ya mipaka ya Dodoma," amesema Mavunde 

 

Aidha Mavunde ameongeza kuwa, "Mashamba haya yakitumika vizuri yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa vikundi vyenu na mimi nitakuwa nanyi bega kwa bega kuwapa msaada wowote unaohitajika ili muweze kufikia malengo yenu, pia nitawasaidia mbegu bora kwa mazao ambayo mtachagua kuyapanda,gharama za maandalizi ya shamba na pia nimezungumza na watu wa TAHA ili baadaye tupate viosk mwendo kwa ajili ya kuuzia mazao yetu,".