Viongozi wa dini wakifanya dua kwa ajili ya Rais Samia
Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa ibada ya swala ya Ijumaa iliyoambatana na dua maalumu ya kumuombea Rais Samia, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Tanga Rajab Abrahaman amesema kwamba ibada hiyo ni muhimu sana katika kipindi hiki.
Kwa upande Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba, ametumia ibada hiyo kuitaka jamii kupambana dhidi ya dawa za kulevya ambapo amesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani Tanga ni lazima yaendelee.
Ibada hiyo inafanyika wakati waislamu duniani kote wakiwa wanasherehekea sikukuu ya Eid Al adha ambayo husherehekewa kila mwaka.