Friday , 30th Jun , 2023

Mishahara ya viongozi kadhaa wa Kenya akiwemo Rais William Ruto, Naibu wake, Rigathi Gachagua, makatibu wa baraza la mawaziri na wabunge itaongezwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Pendekezo hilo limetolewa na Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) ambapo viongozi hao wamepangiwa nyongeza ya mishahara ya asilimia 14 kwa wastani katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Malipo ya jumla ya kila mwezi ya Rais Ruto yatapanda asilimia 7.1 kutoka asilimia 6.7 ya sasa

Kufuatia hatua hiyo inaelezwa kuwa mshahara wa Rais utaongezwe kutoka Ksh.1,433,750 hadi Ksh.1,650,000 na ule wa naibu rais kutoka Ksh.1,227,188 hadi Ksh.1,402,500.