Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Juni 29, 2023, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, ambapo Rais Samia amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mbarouk Salim Mbarouk, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Jaji Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Pia amemteua Balozi Omar Ramadhan Mapuri na Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha Rais Samia amemteua Prof. Idrissa Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), pamoja na Benjamin Mashauri Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi Bw. Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.