
Waziri Chana ameyasema hayo Dar es Salaam wakati akifungua mashindano ya klabu bingwa ya netiboli katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
"Nimepokea taarifa ,nimetoe maelekezo kwa BMT kuhakikisha mnakaa na chama Kisha mniletee mapendekezo ," amesema Dkt Pindi .
Ametoa wito kwa wadau wengine zikiwemo taasisi kuwekeza pia katika ujenzi wa miundombinu ya kimichezo na kugharamia shughuli za michezo hususani michezo ya wanawake pamoja na watu wenye ulemavu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli (Chaneta), Dk Devota Marwa amesema kuwa wataendelea kuratibu programu mbalimbali za maendeleo ya mchezo huo.
"Pamoja na hayo badowanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mdhamini wa kudhamini matukio mbalimbali ya Chama," amesema Dkt Devotha.
Timu 13 shiriki ni pamoja Tamisemi,Jeshi stars,Nyika Queens,Eagle Queens ,JKT Mgulani,JKT Mbweni ,Upendo,NSSF,Polisi Arusha,Kampala,Uhamiaji ,Bukoba Queens na Tanroad