Tuesday , 27th Jun , 2023

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kupitia Shule Kuu ya Biashara kimefanya utafiti maalum kuhusiana na umuhimu wa Uwekezaji kwenye masuala ya Bandari, ambapo wamebainisha kwa lengo la kuzifanya bandari za Tanzania kushindana na Bandari zingine Afrika inahitaji Mwekezaji kutoka nje ya nchi

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mhadhiri Shule Kuu ya Biashara, Idara ya Masoko Chuo Kikuu cha Dar es salaam, David Rweikiza amesema moja ya sababu ya kuruhusu uwekezaji ni kurahisisha utoaji wa meli ndani ya muda mfupi

"Utafiti ulizingatia kuangalia umuhimu wa kuwa na Mwekezaji kwenye Bandari zetu, ambapo tumegundua katika Bandari shindani kama Maputo (Msumbiji) wenzetu Meli kushusha kontena ni masaa 14, Durban (Afrika Kusini) masaa 16, wakati kwetu Bandari inakaa masaa 96" Amesema David Rweikiza

Aidha Rweikiza amesema baada ya kuruhusu Uwekezaji wa Bandari, utasaidia kuongezeka kwa kiasi cha mapato yatokanayo na bandari kutoka Trilioni 7.7 hadi Trilioni 26 kwa mwaka