Tuesday , 20th Jun , 2023

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewataka wazazi na walezi nchini kuongeza juhudi katika malezi na makuzi ya watoto, kutokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa sasa.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mondo, wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma hii leo amesema kuwa watoto wengi wanatia aibu kwa sasa kutokana na kuharibika kimaadili.

Amesema mmomonyoka wa maadili kwa watoto kwa kiasi kikubwa umesababishwa na malezi ya wazazi ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo  na hivyo watoto kuharibika.

Katibu Mkuu Chongolo amesema yakitengenezwa mazingira mazuri ya kuwalea watoto katika maadili kutasaidia kujenga misingi sahihi kwa watoto na hata kwa Taifa na jamii nzima kwa ujumla.