Tuesday , 13th Jun , 2023

Rais Samia amemteua William Lukuvi kuwa mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), ambapo pia ni mbunge wa jimbo la Isimani.

Kushoto ni William Lukuvi na kulia Abdallah Bulembo

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa hii leo Juni 13, 2023, ambapo pia Rais Samia amemteua Abdallah Bulembo kuwa mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bulembo ni mbunge mstaafu

Mwingine aliyeteuliwa ni Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.

Na mwisho amemteua Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.