Tuesday , 13th Jun , 2023

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya lori lenye kontena kufeli na kuparamia wafanyabiashara na kwenda kuingia moja kwa moja kwenye jengo lenye ofisi za michezo ya kubahataisha katika eneo la Yombo Vituka Mwisho wa Lami jijini Dar es Salaam.

Lori likiwa lililoparamia maeneo ya biashara

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hii leo Juni 13, 2023., ambapo lori hilo aina ya Howo lilishindwa kukunja kona na ndipo lilipoparamia baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa katika kona ya eneo hilo 

"Inadaiwa baadhi ya watu wamepata madhara na wamepelekwa hospitalini na tuna uhakika na watu wanne ambao tumewaona kwenye hospitali ya Temeke, na mama mmoja kwa mazingira ya jinsi yalivyo kuna uwezekano mkubwa akawa kwenye hali mbaya na hali yake itategemea jinsi tutakavyopata uthibitisho wa daktari," amesema Kamanda Muliro

Aidha Kamanda Muliro amesema kwamba baada ya dereva wa lori hilo kuona gari limemshinda aliruka kutoka ndani ya gari na kuliacha likienda lenyewe na kupelejkea madhara makubwa yaliyojitokeza.