Sunday , 11th Jun , 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki amesema zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha tano katika Shule za Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Kati vya Serikali Mwaka 2023, limekamilika.

Zoezi hilo limefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka, 2022, kutoka Tanzania Bara. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

Wanafunzi 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na Vyuo vya fani mbalimbali.

(a) Wanafunzi 129,830 wakiwemo wasichana 66,343 na wavulana 63,487 sawa na asilimia 69 ya wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano kwa mchanganuo ufuatao;

(i) Wanafunzi 1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika Shule za sekondari Maalum 8 za Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.

(ii) Wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa ktk shule 519 za Sekondari za Bweni za Kitaifa za Kidato cha Tano

(iii) Wanafunzi 5,044 wakiwemo wasichana 2,515 na wavulana 2,529 wamepangwa ktk Shule 11 za Sekondari za Kutwa za Kidato cha Tano.