Friday , 20th Feb , 2015

Serikali imesema kuwa haijapuuza sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo bali inakwama kutokana na kuwa sekta hiyo inachangamoto nyingi tena zinazohitaji fedha.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

Waziri mkuu Mizengo Pinda ameyasema hayo katika uzinduzi wa mradi wa sayansi teknolojia na elimu ya juu uliopo katika chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa kilichopo katika manispaa ya Iringa.

Amesema kuwa pamoja na kuwa gharama hizo serikali itajitahidi kutatua changamoto hizo kwa kutafuta fedha mahali popote pale pamoja na kukopa benki kuu ili kutekeleza mpango wa kukuza sekta ya elimu.

Hata hivyo amesema kuwa ongezeko la wanafunzi lililopo kwa sasa limechangia sana serikali kuingia gharama kubwa hasa katika suala la miundombinu.

Kwa upande wake waziri wa elimu Dkt Shukuru Kawambwa amesema kuwa changamoto iliyopo katika kutekeleza mradi huo ni ukosefu wa fedha licha ya kuwa serikali inatoa mabilioni ili mradi uweze kukamilika.

Waziri mkuu mizengo pinda ameanza ziara yake katika mkoa wa Iringa kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mkoa na kukagua miradi mbalimbali katika wilaya zote pamoja na kuizindua.