
Coaster iliyopata ajali na kuua watano
Ajali hiyo imetolea Alfajiri ya leo Juni 5, 2023, wakati dereva wa Coster yenye namba T 938 DVQ iliyokuwa ikitokea Mbeya kuelekea Dar-es-Salam kutaka kuyapita magari mengina na kugongana na gari aina Lori lenye tenki ya mafuta T 693 DMF -T 586 CKR iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro ACP Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema wanamtafuta dereva wa Coaster ambaye amesababisha vifo vya watu hao na majeruhi.
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya St.Kizito Mikumi mkoani humo Steven Mbilinyi, amesema tayari wamepokea miili ya watu 5 wanaume 3 na wanawake 2 na majeruhi 20.