
Wakazi wa mtaa huo wamesema majira ya saa moja asubuhi wakati watoto wao wakienda shule waliona kichanga hicho ndipo wakawajulisha wazazi wao ambao walienda na kukiangalia na kukuta kichanga hicho tayari kimeshapoteza Maisha
Bado haijafahamika mara moja ni nani ametupa mwili huo katika eneo hilo huku diwani wa kata ya kitangiri ulipo mtaa huo wa kileleni akisema baada ya taratibu za polisi kufanyika watalazimika kuuzika mwili wa kichanga hicho
Stella Kilawe ni afisa mtendaji wa mtaa wa Kileleni amesema kitendo hicho cha kutupa kichanga siyo kizuri na kutoa ari kwa wakazi wa mtaa huo na mitaa Jirani kuacha tabia hiyo