Thursday , 18th May , 2023

Wananchi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, wameiomba serikali iwapatie chakula cha msaada bure kwani kwa sasa wana adha kubwa ya njaa iliyosababishwa na Tembo kula mazao yao yote shambani

Wamesema kutokana na maisha yao kutegemea zaidi kilimo, kwa sasa wanapitia changamoto kubwa kwasababu Tembo wamekula mazao yao shambani

Kwasasa serikali imewapatia chakula cha msaada kwa bei nafuu lakini wao wanasema hawawezi kumudu gharama hiyo hivyo wanataka wapatiwe bure

"Hatuna pesa ya kununua chakula cha msaada, vyakula vinakuja na bei shilingi 800 na sisi maisha yetu tunategemea kilimo huku tembo wamekula mazao yote, tutatoa wapi hela ya kununua vyakula vya msaada?" Khadija Mohamed, Mwananchi Nachingwea

"Chakula sina, na hela ya kununulia chakula sina, tunakuagiza mkuu wa wilaya, tupate walau kilo saba za bure" Hassan Ally, Mwananchi wa Nachingwea

Akisikiliza hoja za wananchi wilayani mwake, Mkuu wa wilaya ya Nachingwea amewataka wananchi kupunguza ghadhabu na kukiri serikali kuifahamu kadhia hiyo.