Akizungumza na East Africa Radio, Mratibu wa semina ya waalimu wa michezo Mkoa wa Dar es salaam, Adolf Ally amesema mchezo huu ni mpya ambapo katika Afrika ni nchi tatu ndizo zinashiriki mchezo huu mojawapo ikiwa Tanzania hivyo wanamichezo wa mchezo huu wanatakiwa kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchuakua mafunzo ya mchezo huu.
Ally amesema, semina hiyo itakuwa endelevu kwa nchi shiriki za mchezo huo ambapo itaenea katika maeneo yote ya Dar es salaam.
Kwa upande wake, Mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Salma Pontiya amesema, wanaamini walimu wote wanaishiriki semina hii itasaidia kutoa elimu ya mchezo huu kwa watoto walioko mashuleni na kuweza kuukuza mchezo huu hapa nchini kupitia mchezo huu.
Semina hiyo inatarajia kuendeshwa kwa muda wa wiki moja ikisimamiwa na Rais wa Chama chya kuruka kamba Duniani Shaam Hamilton.