Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Fred Enanga, akiwa na mashabiki wa Arsenal
Januari 22, 2023, mashabiki wa timu hiyo mjini Jinja nchini Uganda, walikamatwa na polisi baada ya kuanzisha gwaride la kushangilia ushindi wa mabao walioupata dhidi ya Manchester United.
"Nimewashauri mashabiki wa Arsenal mjini Jinja kuwashirikisha polisi mapema katika kusherehekea kwao endapo watapata ushindi dhidi ya Manchester United ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote kwenye harakati zao za ushangiliaji," amesema Enanga.