Wanaoshikiliwa ni mfanyakazi wake wa ndani (House Girl), Mama wa mfanyakazi huyo pamoja na ndugu mmoja wa mfanyakazi huyo
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani
Polisi wamesema katika msako wamemkuta mfanyakazi huyo wa ndani akiwa na vitu mbalimbali vya marehemu ikiwemo hereni, pete na vitu vingine vya thamani
Mwili wa Hamida ulikutwa Jumanne Novemba 29, 2022 nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umelala sakafuni kifudifudi ukiwa na mtandio shingoni mwake huku mfanyakazi wake wa ndani ambaye alikuwa akiishi hapo akiwa ametoweka