Monday , 21st Nov , 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki  ametaja kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza  katika wilaya ya urambo mkoani Tabora

Akiwa katika mwendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Tabora ya kukagua ujenzi wa madarasa andalio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 ,amesema kasi ujenzi wa madarasa hayo katika  wilaya ya urambo haiendani na muda elekezi wa kukamilisha mradi huo

Ameagiza ujenzi huo kufanyika usiku na mchana ili kuendana na muda wa wanafunzi  wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kuanza masomo yao  hivi karibuni.