Monday , 7th Nov , 2022

Imeelezwa kuwa hati fungani zilizoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam imeongezeka kwa shiling bilioni mbili kutoka shilingi trilioni 16.65 kwa wiki iliyoishia mwezi oktoba hadi kufikia trilioni 16.67 ukubwa wa mtaji sokoni ukipungua kwa asilimia 0.44

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa katika robo ya nne ya mwaka mpaka sasa wawekezaji wa ndani wamechangia 93.93 ya uwekezaji huku wa nje wakichangia asilimia 6.07 ya uwekezaji.

Aidha miamala iliyofanyika kwenye upande wa hatifungani ni thamani ya shilingi 52.42bilioni sawa na ongezeko la asilimia 163 ikilinganishwa na miamala yenye thamani ya shilingi bilioni 21 .05 kwa wiki iliyoishia oktoba