Onesho hilo ambalo litafanyika usiku wa tarehe 14/2/2015 ambayo itakuwa siku ya wapendanao, limeandaliwa na kampuni inayokuja kwa kasi kwenye mambo ya burudani inayojulikana kwa jina la King Solomon Events, na kudhaminiwa na East Africa Television na East Africa Radio.,
Kwenye tamasha hilo burudani mbalimbali zitatolewa kutoka kwa Ben Pol na Bi. Paticia Hilary, pamoja na msanii mwenye sauti ya kipekee Grace Matata.
Pamoja na hayo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa watu watakaokuja kuburudika wakiwa na wenzi wao, ikiwemo pete iliyotengenezwa kwa madini ambayo yanapatikana Tanzania pekee ya Tanzanite, yenye thamni ya shilingi milioni 4 za kitanzania.
Zawadi nyingine ni vocha yenye thamani ya shilingi laki mbili, ambayo itatumika kulipia chakula kwenye mgahawa wa chakula.
Msanii Ben Pol ataimba nyimbo zake ambazo zinafanya vizuri zenye ujumbe wa upendo, pamoja na za wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
