Wednesday , 4th Feb , 2015

Mwigizaji maarufu wa filamu ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Tanzania H-Baba hivi sasa ameufungua mwaka kwa kuandaa project yake mpya ikiwa ni wimbo mpya alioubatiza jina 'SHOWTIME'.

Msanii wa muziki wa bongofleva nchini H-Baba

H-Baba ambaye hivi sasa ni mzazi mwenye majukumu ya kuitunza familia yake amesema kuwa audio ya wimbo huo imefanyika katika studio mpya kabisa inayoitwa Fadhaget Music iliyopo huko Mbezi Beach Afrikana chini ya mtayarishaji mkubwa 'Mkolinto'.

Aidha, mkali huyo mwenye kulimiliki vyema jukwaa awapo stejini amesema kuwa video ya wimbo huo mpya 'SHOWTIME' unatarajiwa kuanza muda si mrefu na kusema kuwa ataachia pamoja na audio ili visipishane sana huku akiweka siri ya kutosema ataifanya na nani kazi hiyo mpya.