Wednesday , 4th Feb , 2015

Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba na Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji Mijini, kwa miji 26 nchini, ili kuzibana mamlaka hizo ziweze kuwapatia wananchi maji kwa wakati na kuondoa kero ya upatikanaji wa maji mijini.

Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji

Akiongea mara baada ya kutiliana saini Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe amewaagiza wakuu hao kwenda kwa kasi kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji bila kipingamizi.

Awali akimkaribisha kufungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Chiku Galawa amesema kwa niaba ya wananchi kuwa, wananchi wana matarajio makubwa kupitia mikataba hiyo.

Aidha amewataka wakuu hao kubaini vyanzo vya maji, kama uvunaji wa maji ya mvua, watu wanaoishi kwenye vyanzo vya maji kutopatiwa huduma hiyo hali inayozua migogoro kati ya wananchi na mamlaka za maji.