Tuesday , 3rd Feb , 2015

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha kimetishia kuwafukuza uanachama viongozi wake wanaoanza kutengeneza makundi ya uchaguzi badala ya kushughulikia matatizo ya wananchi.

Chama  cha Mapinduzi  (CCM) mkoani  Arusha  kimetishia   kuwafukuza   na  kuwafuta  uanachama  viongozi   wake  wanaoanza  kutengeneza  makundi   ya  uchaguzi  badala  ya  kushughulikia  matatizo  ya   wananchi,   tatizo  ambalo  limeshaanza   kuleta  dalili  za  kukigawa  chama  hicho.

Akizungumza  na   wananchi   wa  maeneo  mbalimbali  katibu  wa chama  hicho  mkoa  wa Arusha  bw,  Alfonce  kinamhala   amesema  wapo  viongozi  na  wanachama  ambao   badala  ya  kujishughulisha   na  matatizo  ya  wananchi  na  kutekeleza  ilani   ,wanatumia  muda  wao   kupanga  makundi  na  kujiandaa  kugombea  nafasi   jambo  ambalo  chama  hakiwezi   kulifumbia  macho.

Baadhi ya viongozi  wa  wilaya   akiwemo  mwenyekiti wa  CCM  wilaya  ya  Monduli   Reuben Olle  Kuney  wamesema  tatizo  hilo  lipo   na  ni kubwa  zaidi   katika   ngazi  ya  kata  na  kwamba  limejitokeza  wazi  wazi   wakati  wa  chaguzi  za  serikali  za  mitaa.

Kwa   upande  wao   baadhi  ya  viongozi   wa  kata    wanaotuhumiwa   wamewalaumu    viongozi   wa  ngazi  za  juu   za  chama  hicho    kuwa  ndio  wanaosababisha  matatizo   yaliyopo   sasa   likiwemo  la   kuondoa  majina  ya wagombea wanaopendekezwa  na  wana nchi na   kuweka   watu   wao  .

Baadhi   ya  wananchi   wakiwemo     wa  wilaya  ya Monduli   wamesema  pamoja  na  chama  hicho kutekeleza   ahadi  zake   kwa  kiasi  kikubwa,   kasi  ya  utendaji  wa  viongozi  wake  imekuwa  ikipungua  siku hadi  siku   kadri   muda  wa  uchaguzi  unavyokaribia