
Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto
Kenya imezindua mpango wa kuchochea ongezeko kutokana na sekta ya viwanda Rais Ruto amesema Kenya itapanua sekta yake ya viwanda kupitia kushauriana na kubadilishana mawazo na kwenda pamoja kama taifa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanaviwanda ya Kenya (KAM) Bw. Rajan Shah, amesema kuna maeneo manne yenye fursa ya kuiwezesha Kenya kufikia lengo hilo, ambayo ni nguvu ya ushindani duniani, ongezeko linalolenga uuzaji nje wa bidhaa, kuifanya sekta ya kilimo kuhusiana na viwanda na kuendeleza makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati.