
Akitoa taarifa ya mwenendo wa soko la la hisa la Dar es salaam Afisa maendeleo ya Biashara DSE Leonard Kameta amesema kushuka Kwa thamani ya soko Hilo kumesababishwa na kushuka Kwa bei za hisa katika kampuni za NMG,KCB,EABL na JHL
Katika robo ya nne ya mwaka mpaka Sasa wawezekaji wa ndani wamechangia asilimia 98.14 ya uwekezaji wote huku wawezekaji wa nje wakichangia asilimia 1.86 ya uwekezaji
Katika wiki iliyoishia Octoba 13 miamala iliyofanyika kwenye upande wa hatifungani ina thamani ya shilingi bilioni 28.30 ikikinganishwa na miamala yenye thamani ya shilingi bilioni 120 Kwa juma lililoishia Octoba Saba