Wednesday , 19th Oct , 2022

Kampuni ya Magic Builder's International ltd inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ujenzi ikiwemo bidhaa ya White skim wall putty imeandaa mkutano mkubwa wa mafundi katika Jiji la Dar es Salaam ikilenga kuwapa elimu juu matumizi ya bidhaa hizo Ili kuongeza weledi.

Rai hiyo imetolewa na Mwakilishi wa kampuni hiyo na Mtendaji Mkuu kwenye sekta ya uwekezaji ambapo amesema wameamua kufanya mkutano huo Nov 20,2022 mlimani city Ili kufungua fursa zaidi

Hata ivyo hii Leo kampuni hiyo imeamua kuwatangaza wasanii mbalimbali na kuingia nao makubaliano kama mabalozi ambao watashirikiana nao kutangaza bidhaa zao ikiwemo white skim wall putty.