
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde, akiwa mkoani Mwanza katika Kongamano la wanawake wa ushirika wa akiba na mikopo Tanzania na kueleza ipo haja ya vyama vya ushirika kuwekeza katika uzalishaji wa mazao hayo muhimu ambayo uhitaji wake ni mkubwa.
Wanachama wa ushirika wameeleza watachukua hatua kuwekeza katika maeneo yenye fursa zaidi za kukuza uchumi ikiwemo kilimo.