
Wafanyabiashara wilayani Nyang'hwale, wakipewa elimu
Akitoa elimu kwa wafanyabiashara hao, Afisa Elimu na huduma kwa mlipakodi mkoa wa Geita Justine Katiti, amesema wafanyabiashara wengi wamekuwa wakikosa fursa za kufanya biashara na wadau mbalimbali kwa kuwa hawajajisajili TRA, pia kutojisajili kumewakosesha fursa za mikopo kwenye taasisi za fedha.
"Wafanyabiashara tukiweka kumbukumbu sahihi za biashara zetu na kutoa risiti kwa kila mauzo tunayofanya tutakadiriwa na kulipa kodi stahiki, tutaondoa malalamiko ya kodi, biashara zetu zitazidi kupanuka na serikali itakusanya mapato yake na hivyo kutoa huduma bora zaidi na haraka kwa wananchi wake," amesema Katiti