
Pichani ni baadhi ya watumishi wa CRDB Benki wakipokea tuzo
Tuzo hiyo ya ‘Global Finance’ ambayo imetolewa baada ya vikao vya benki ya dunia Jijini Washington DC Marekani, imepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiambatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Benki hiyo.
“Tuzo hii tumeipokea kwa furaha kwasababu ni heshima kwetu kama benki, lakini hii ni matokeo ya mahusiano mazuri na ya kimkakati tuliyonayo na taasisi mbalimbali za kifedha. Tunawashukuru sana wateja wetu kwani wao ndio wanaifanya CRDB iwe benki bora Tanzania, wawekezaji walioiamini benki yetu na kuweka fedha zao wote wamekuwa sehemu 8ya mafanikio hayo. Lakini pia tunawaahidi wateja wetu kuendelea kuwapatia huduma bora na bunifu"- Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB Bw. Nsekela, anaweka bayana kwamba sera nzuri za serikali katika uchumi na uwekezaji zimeifanya benki hiyo kupata tuzo hiyo.
Hii ni tuzo ya pili ya ‘Benki Bora Tanzania’ kwa Benki ya CRDB ndani ya mwaka huu baada ya kutunukiwa tuzo kama hiyo na jarida maarufu la fedha na uchumi la nchini Uingereza la ‘Euromoney’ mwezi Julai.