Monday , 2nd Feb , 2015

Wafanyabiashara na baadhi ya wamiliki wa viwanda mkoani Mara wamelalamikia mfumo mbaya wa soko la bidhaa katika nchi jirani ya Kenya kwa kuweka vikwazo katika uuzaji wa bidhaa.

Wafanyabishara wakiwa katika kikao cha pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wafanyabiashara   na  baadhi  ya wamiliki   wa   viwanda  mkoani  Mara wamelalamikia  mfumo  mbaya  wa  soko  la  bidhaa  katika  nchi  jirani  ya  Kenya  kwa  kuweka  vikwazo  katika  uuzaji   wa  bidhaa  hatua  ambayo  imekuwa  ikisabisha kero  kubwa katika uuzaji  wa  bidhaa  hizo   zikiwemo  za  maziwa   katika  nchi  hiyo.

Wakizungumza na ujumbe  wa  wizara  ya  ushirikiano  wa  Afrika  Mashauriki ukiongozwa  na naibu katibu  mkuu  wake  Amantius  Msole, wafanyabiashara  hao  wamesema  kuwa  licha  ya  vyombo  vya  dola  nchini humo  kuweka  vikwazo  katika uuzaji  wa  bidhaa  nchini  humo, wameiomba  serikali  kupunguza  kodi  kama  zilivyo  nchi  wanachama  hasa   katika bidhaa  ya  maji safi  ya  kunywa  ili  kuwezesha  bidhaa  hizo  kushindana  katika  soko.
 
Hata  hivyo  naibu  katibu  mkuu  wa  wizara  ya  ushirikiano  wa  Afrika  Mashariki Amantius  Msole, amesema  lengo  la  ziara  hiyo  katika  maeneo  ya  mipakani  ni kuona jinsi   watanzania  wanavyonufaika  na fursa ya soko  la  pamoja  na  changamoto zinazowakabili  ili ziweze kupatiwa  ufumbuzi.