Friday , 14th Oct , 2022

Wafanyabiashara wa Nishati ya mkaa katika soko la Magomeni wamesema serikali ndiyo yenye uwezo wa kudhibiti bei ya mkaa ambayo inapaa juu Kila kukicha.

Kwa takribani Miezi kadhaa sasa Nishati hii imekuwa ikipanda bei Kwa guni kutoka kununua gunia Moja Kwa elfu 38 hadi sasa kununuliwa Kwa Shilingi elfu 55 hali inayofanya sasa gunia Moja kuuzwa Hadi Shilingi elfu 65 Kwa bei ya reja reja.

Hali hiyo inatajwa kuchagizwa na changamoto nyingi ikiwemo ushuru, gharama za juu za uzalishaji Toka Kwa porini ulipaji wa vibali hivyo kuzasabisha gharama ya gunia kupaa juu.

Upandaji wa bei ya mkaa umetajwa kuwaumiza wananchi wengi Kwa kuwa hutumiwa zaidi na wenye kipato Cha chini hivyo kuiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwenye biashara hii.

Biashara ya mkaa Kwa sasa imekuwa ikipata ushindani mkubwa tangu kuliporipotiwa na kuanza kutumika Kwa gesi asilia nchini Tanzania.