
Atupele Mwakibete-Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.
Maadhimisho haya ya wiki ya usalama wa reli ni ya kwanza kufanyika nchini Tanzania tangu kuatangazwa na kufanyika Kila nchi za SADC ambapo Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema hatua za ujenzi wa reli ya kisasa Kwa hatua zote umekwisha tumia fedha nyingi hivyo kuwataka wataalamu na watumishi kuwa waadilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo kwneye maeneo mbalimbali akitumia dakika Moja pia kuwakumbuka wote waliofikwa na ajali za usafiri treni kugonga ama kugongwa.
"serikali imeweka pesa nyingi sana kwenye mradi wa SGR tunataka wale wenye tabia ya kufanya shughulimbali mbali pembezoni mwa reli kwanza ni hatari kwa usalama wao lakni pia wanaharibu miundo mbinu niwaombe TRC nawadau wote wa usafirishaji kukemea na kuchukua hatua kali"amesema Atupele Mwakibete-Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.
Aidha amesema Ili kulinda miundombinu ya reli shughuli zote za kiuchumi zisifanyike kwenye maeneo ya reli akiwataka pia kuwataja wananchi wenye tabia ya kuhujumu miundombinu hiyo
Aidha Katika kuadhimisha wiki hii ya usafiri wa reli tunaendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya usafiri huu pamoja na usafiri wa treni ya haraka ya SGR Ili keupuka Athari nyingi za ajali zinazotokea.
Usafiri wa reli unatajwa kuwa rahisi wa uhakika na wenye gaharama nafuu kuliko usafiri wowote ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho haya Kwa mwaka huu inasema chukua tahadhari treni Ina mwendo Kasi lakini husimama pole.