Wednesday , 12th Oct , 2022

Imeelezwa kuwa moja ya changamoto ambayo imekwamisha kwa kipindi kirefu sekta za uzalishaji kukua ni kutofungana kwa sera za nchi baina ya sekta na hali ambayo imesababisha kuzorota kwa sekta za uzalishaji.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe,

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe, katika majadiliano ya pamoja na watalaamu wa uchumi na kisera kutoka nchi 11 pamoja na washirika wa maendeleo kutoka Umoja wa Mataifa ambapo ishu za kutofungamana kwa sera, changamoto za uzalishaji duni kwenye sekta za kilimo zinakwamisha viwanda ambavyo ndiyo azma ya serikali.

Amesema kwa ishu ya uzalishaji nchini imekuwa nyuma kwa kipindi kirefu ambapo sasa wanahuhisha baadhi ya sera ziendane na wakati uliopo.

Hata hivyo watalaamu kutoka mashirika binafsi, wataalamu wa utafiti wamebainisha changamoto nyingi ziko kwenye sekta ya Kilimo, viwanda, ujenzi, sukari na mafuta ya kula.

Mkutano huo umebainisha matatizo mengi ya Afrika ni umaskini hivyo kuja sasa na sera na mikakati ya kuinua uchumi ukiwemo mradi huo ambao umeanzishwa tangu mwaka 2020 Tanzania ikiwa ni mnufaika.