Monday , 10th Oct , 2022

Baadhi ya masoko yaliyotengwa yatumike na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga katika manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametajwa kutelekezwa na wafanyabiashara hao na kurejea tena kuendesha biashara zao maeneo yasiyo rasmi ya pembezoni mwa barabara ambayo yanatishia usalama wao.

Wafanyabishara wakiwa Mwanza

Hayo yamebainishwa na  na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala wakati akizindua Saccoss ya SHIUMA Ilemela ya wafanyabiashara wadogo ikilenga kuwezesha kundi hilo kupata mitaji yenye masharti nafuu.

Kwa upande wao wafanyabiasha hao wadogo wameeleza uanzishwaji wa Saccos ya SHIUMA Ilemela kwamba utawasaidia kufikia malengo yao ya kibiashara pamoja na kutoa  wito kwa wengine kujiunga.

Aidha akifafanua kuhusu kundi hilo kurejea barabarani  Mwenyekiti wa Shirikisho la wamachinga Mkoa wa Mwanza Mohamed Dauda amesema ushirikishwaji katika maeneo wanayo pelekwa ndio suluhisho.