
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Hilda Bujiku amesema tozo zimesababisha miamala ya simu kushuka upande wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na vile vile upande wa kutoa pesa kwa wakala kwa zaidi ya asilimia 30.
Kuhusu taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na waziri wa fedha akiwa bungeni kwamba tozo za miamala ya fedha zitapunguzwa kwa asilimia 10 mpaka 50 amesema inatia moyo kwao kama wawekezaji kwenye sekta ya mawasiliano kwa sababu ni kitu wamekuwa wakikisubiri.