Friday , 9th Sep , 2022

Vijana 130 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wamefanikiwa kupatiwa elimu ya ujasiriamali pamoja na namna ya kujiajiri kwenye sekta ya viwanda

Baadhi ya vijana waliopatiwa mafunzo

Vijana hao wamefanikiwa kupatiwa elimu kupitia mradi wa uanagezi ambapo mradi huo uliibuliwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia na kudhamiwa na Benki ya Dunia huku ikiratibiwa na SIDO.

Mara baada ya kufungua mradi wa uanagezi ambao umewakutanisha wamiliki,pamoja na vijana wajasiriamali mkoa wa Arusha meneja wa SIDO mkoa wa Arusha Jafari Donge, amesema kuwa mradi huo ulidumu kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Donge alisema kuwa SIDO kupitia kwenye mradi huo umeweza kuibua ajira mpya kwa kuwa vijana hao waliweza kupelekea kwenye viwanda mbalimbali ambavyo vinatekeleza majukumu Yao ya kiujasirimali.