
Kundi hilo limethibitisha kupitia mtandao wake wa kijamii tawi la Msumbiji. Vyombo vya habari nchini humo viliropoti siku ya jana kwamba mtawa huyo raia wa Italia mwenye umri wa miaka 83 aliyejulikana kwa jina la Sister Maria De Coppi, alipigwa risasi na kupoteza maisha wakati vikosi vya kijihadi vilipovamia kijiji cha Chipene katika wilaya ya Memba .
Katika shambulizi hilo watu kadhaa wanaripotiwa kuchinjwa na vikosi hivyo.
Katika madai yao IS wamesema kwamba wameamua kumuua sister huyo sababu anaeneza sana dini maeneo hayo.
Vikosi hivyo pia vilichoma moto kanisa , magari mawili pamoja na mali zingine zilizokuwepo kwenye eneo hilo.
Nje ya tukio hilo, kundi hilo la IS limekiri kuhusika na tukio ambalo lililofanyika mwezi June mwaka huu huko Nampula katika kijiji cha Memba na kuwachinja watu.
Eneo la Nampula linapatikana kusini mwa jimbo la Cabo Delgado ambapo shuguli za IS zinasemekana kuchukua hatamu. Rais wa Msumbuji Filipe Nyusi amethibitsiah uwepo wa matukio hayo.
