Tuesday , 27th Jan , 2015

Star wa filamu na vichekesho wa kimataifa kutoka Canada, Russel Dominic Peters anatarajiwa kutua nchini Kenya, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kabisa barani Afrika itakayofanyika terehe 8 mwezi Februari.

Mchekeshaji nyota wa nchini Canada Russel Dominic Peters

Katika wakati wake nchini Kenya, Peters anatarajiwa kukutana na wachekeshaji maarufu wa nchi hiyo akiwepo Eric Omondi na Churchill ambapo watapata nafasi ya kushiriki katika jukwaa moja kuchekesha.

Star huyu tayari amekwishathibitisha juu ya ujio wake huu mkubwa Afrika kwa njia ya mtandao ambapo tayari wadau mbalimbali hususan wale wa fani ya vichekesho wameonesha matarajio ya kujifunza mengi kutoka kwa msanii huyu wa kimataifa.