
Amesema hali hiyo huchangia wafugaji kuendelea kuwa maskini kutokana na nyama kukosa soko.
Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya wakulima - Nanenane - Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa ili kuhakikisha inapatikana nyama laini na yenye soko lazima elimu itolewe kwa jamii kuanzia ngazi za chini hadi za juu.
"Jamii iache kufunga ng'ombe kwa stress, ng'ombe anatembea kutoka pori la Karagwe hadi Ngara, kesho wamchinje lazima nyama yake iwe ngumu" amesema Chalamila.